Lissu Afunguka Kasoro za Kisheria Alizofanya Makonda Wakati wa kutangaza Wahusika wa Madawa ya Kulevya,Adai Huenda Kesi Ikamgeukia Yeye Mwenyewe..!!!

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ametaja kasoro kadhaa katika zoezi la vita ya dawa za kulevya lililoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda. 

Amesema, 
Kwanza, Mkuu wa Mkoa hana mamlaka yoyote ya kuelekeza watu kwenda kuripoti polisi. Hii ni licha ya mamlaka yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na mamlaka yake ya kipolisi yapo chini ya Sheria ya Tawala za Mikoa. 

Pili, kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Jinai, kila mtu ana wajibu wa kutoa taarifa ya kosa la jinai analoona limetendeka kwa polisi. Hii ni ile inayoitwa kufungua RB. Mkuu wa Mkoa Makonda alitakiwa afungue RB kwa wote anaowatuhumu kufanya biashara ya madawa. Hajafanya hivyo na ni kosa la jinai kutokufanya hivyo.

Tatu, kwa kutumia mamlaka yake ya kipolisi, Mkuu wa Mkoa Makonda alikuwa na uwezo wa kuamuru wale wote anaowatuhumu kufanya biashara ya madawa kukamatwa na kuwekwa kizuizini kwa masaa 48 na baadae kufikishwa mahakamani. Badala ya kuamuru ‘wahalifu’ hawa wakamatwe, Mkuu wa Mkoa Makonda aliwaelekeza wajipeleke polisi kwa mahojiano.

 Nne, kwa kuzingatia hatari kubwa ya madawa ya kulevya kwa jamii yetu, sheria husika za nchi zimeweka adhabu ya chini kabisa ya kifungo cha miaka 20 kwa wanaothibitika na mahakama kuhusika na biashara hiyo. Aidha, makosa ya madawa ya kulevya hayana dhamana kisheria. Iweje wale wote waliotuhumiwa na Mkuu wa Mkoa Makonda wamepelekwa mahakamani lakini wote wamepewa onyo tu au wamepewa dhamana Mahakamani. 

Kati ya mapolisi 11 waliotuhumiwa, hakuna hata mmoja aliyepelekwa mahakamani na kushtakiwa kwa tuhuma hizi. Badala yake, tunaambiwa wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa polisi dhidi yao. Kwa mujibu wa Sheria zetu za ajira, mtumishi anayesimamishwa kazi analipwa mshahara kamili kwa muda aliosimamishwa 

Tano, kitendo cha kuwatangaza watuhumiwa kwa namna alivyofanya Mkuu wa Mkoa Makonda, kesi yoyote itakayofunguliwa dhidi yao itaharibika. Kila mtuhumiwa atajitetea kwamba amekamatwa na kushtakiwa kwa sababu za kisiasa na kwa amri haramu za Mkuu wa Mkoa. Kila mtuhumiwa atajitetea kwamba hakuna RB yoyote iliyofunguliwa dhidi yake na kila wakili wa utetezi atataka Mkuu wa Mkoa Makonda aitwe mahakamani kwa ajili ya kuhojiwa. Makonda ataliwa nyama na mawakili kwenye cross-examination. Kwa kifupi, hii sio vita dhidi ya wauza ‘unga’, hii ni political charade na character assassination inayofanywa kwa mbinu za ovyo kabisa bila kufuata sheria Haitafika popote.

from Blogger http://ift.tt/2kWKCEO
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment