MAHAKAMA KUU PAKISTANI YAPIGA MARUFUKU KUSHEREHEKEA VALENTINE

Katazo hilo linazuia kuweka matangazo au ujumbe wowote ule unaohusiana na sherehe hizo kwa njia ya mtandao au kwenye karatasi, linazuia kufanya biashara yoyote inayohusiana na sherehe hizo na kusisitiza kuwa si ruhusa kusherehekea siku hiyo “katika sehemu yoyote ya umma au kwenye jengo lolote linalomilikiwa na serikali.”
Mahakama hiyo imeitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Vyombo vya Habari za Mtandaoni nchini Pakistan (PEMRA) kufatilia vyombo vyote na kutoa taarifa juu ya ukiukwaji wa aina yoyote ile juu ya katazo hili.
Uamuzi huu wa Mahakama Kuu umetolewa kutokana na maombi yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na mwananchi anayeitwa Abdul Waheed ambaye alidai kuwa matangazo yanayoendelea sasa kuhusu sherehe za siku hii ya wapendanao “yanakiuka mafundisho ya dini ya Uislam na kwamba inatakiwa ipigwe marufuku mara moja.”
Mgogoro kuhusu Siku ya Wapendanao
Nchini Pakistan, siku ya ‘wapendanao’ inaonekana kwa baadhi kuwa ni sawa kuisherehekea na kwa wengine inachukuliwa kama kuukaribisha utamadauni wa nchi za magharibi.
Kwa wale wanaopinga pia wana hoja zao, si jambo la kushangaza kuona ikipigwa vita. Makundi mbalimbali ya kidini kama chama cha siasa cha kiislamu kinachoitwa Jamat e Islami kimapinga mara kadhaa juu ya nchi hiyo kuiweka siku hii katika siku za sherehe zinazotambuliwa nchini humo na kila mwaka huwa wanaandaa makongamano wakipinga sherehe hizo zinazofanyika tarehe 14 mwezi wa pili.
Mwaka 2016, sherehe hizi zilipigwa marufuku pia na serikali ya mtaa katika jiji la Peshawar, lililopo Kusini mwa kanda ya Khyber Pakhtunkhua.
Rais wa nchi hiyo Mamnoon Hussain, alitoa tamko mwezi wa pili mwaka jana akiwataka raia wa nchi hiyo kutosherehekea siku hiyo kwakuwa “si katika tamaduni za Uislamu, ila ni tamaduni za Magharibi.”
Uamuzi wa Mahakama Kuu ya jijini Islamabad pia umewagawa watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini humo, ambapo wapo wanaounga mkono marufuku hiyo na wengine wakionesha kupinga.
Fursa ya kufanya biashara
Ingawa siku hii haina mashabiki wengi nchini humo, kwa miaka ya hivi karibuni, baadhi ya kampuni zimekuwa zikitumia sikukuu hiyo kama fursa ya kutangaza na kukuza biashara zao.
Mohammad Naveed anamiliki duka la maua kando ya barabara anasema amewekeza zaidi ya shilingi milioni nnekununua maua ili ayauze siku hiyo
Katika wiki ya kwanza ya mwezi Februari, wafanyabiashara walianza kuuza maputo yenye umbo la moyo na kupandisha bei kwa mawaridi mekundu.
Katika masoko ya jijini Islamabad leo Jumatatu, wauza maua waliokuwa wamesimama huku wameshikilia mawaridi makubwa waliyoyatengeneza kwenye umbo la moyo wameonekana wakiwa na wasiwasi mkubwa juu ya hatma ya biashara zao kutokana na marufuku hiyo iliyotolewa na Mahakama Kuu nchini humo.
“Tumetumia siku nne au tano kutengeneza maua haya, mimi nina maua ya aina hii arobaini ambayo nategemea niyauze kesho,” alisema Sultan Zaib.
Wauza maua huyapata maua hayo katika mashamba ya mji wa Punjab uliopo mbali kidogo na jiji hilo. Kwa kawaida wanafanya mauzo ya karibu shilingi 170,000 kwa siku lakini mauzo yao huongezeka mara kumi zaidi ya hapo siku ya wapendanao inapofika. “Wakisimamia marufuku hii na tukashindwa kuuza maua haya itatusababishia hasara kubwa sana,” alisema Naveed.
Mamia ya maharusi wakisubiri kwenye mstari ili wafungishwe ndoa ya pamoja jijini Manila, Ufilipino

from Blogger http://ift.tt/2lFB5VA
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment