Ushawahi kujiuliza kile kipira cha mviringo kwenye chaja yako kazi yake? kama hujawahi kukiona, angalia chaja yako hapo utakiona kitu cha mvilingo. Kinaonekana kama kitu ambacho hakina kazi lakini bila hicho kidubwana, laptop yako inaweza isifanye kazi.
Hicho kifaa kinaitwa Ferrite Bead. ni kifaa ambacho kinapunguza mawimbi makali ya sauti katika vyombo vya umeme.
Kifaa hicho kinazuia laptop kupatwa na mawimbi ya umeme ambayo yanakuwa kama mikwaruzo ya sauti inayotokea kwenye nyaya au sauti zinazotoka kwenye converter za AC-DC au AC line.
Mara nyingi kifaa hiki kinafungwa kwenye chaja za laptop na vyombo vingine kama printer, ila huwezi kukikuta kwenye chaja za simu. Hii ni kwa sababu simu na vifaa vingine vya mkononi kama tablets huwa vimetengenezwa kwa vifaa ambavyo vinaweza hamishika na vinavyofanya kazi kwa pamoja, japo kuwa vinatengeneza hayo mawimbi ya sauti.
kifaa hiki kimetengenezwa na matilio ya iron oxide yenye usumaku. Ambapo kinafyonza au kutoa miale wakati umeme ukipita. Bila hicho kifaa muingiliano mkubwa wa vifaa vilivyokuwa karibu unaweza tokea kwa mfano speaker hua zinatoa mikwaruzo ya sauti ukiweka karibu na simu hiyo inafahamika kama ‘electromagnetic interference.’
Je? kunamatumizi mengine unayofahamu ya kifaa hiki ambayo sisi tumesahau unaweza ukayaandika hapo chini kwenye komenti.
from Blogger http://ift.tt/2lLeq7h
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment