Asma Juma, mzazi aliyejifungua watoto mapacha na kudai kuibiwa mtoto mmoja katika hospitali ya Temeke, amefunguka kuelezea kilichotokea.
Mzazi huyo anawatuhumu wauguzi wa hospitali hiyo kumuiba mtoto wake huyo akidai, awali wakati alipokuwa na ujauzito picha za Ultrasound alizowahi kupima zilionyesha kuwa ana ujauzito wa mapacha na hata alipokuwa hospitalini hapo alimsikia nesi aliyekuwa akimuhudumia akithibitisha kua ana watoto wawili.
Akiongea na kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, Asma amesema, “Wakati nipo chumba cha upasuaji, baada ya kuambiwa nafanyiwa operesheni, yule nesi aliyekuwa ananihudumia akiwa na mtu mwingine nilimsikia akisema ‘viko viwili’ akimaanisha wako watoto wawili, yule nesi aliniambia nisijitingishe, baadaye walinichoma sindano nikapoteza fahamu.”
“Nilivyozinduka nikajikuta nipo chumba cha pili nikiwa nasikia maumivu makali sana, niliwaomba dawa wakaniambia nitazikuta wodini hapo hakuna dawa za maumivu. Nilifanyiwa operesheni saa nane hadi saa kumi na mbili ndipo nikapelekwa wodini, kwa muda wote huo sikupewa watoto wangu. Nimeletewa mtoto mmoja saa kumi na moja alfajiri nakumbuka wakati nipo wodini nilimsikia yule nesi aliyekuwa akinihudumia akisema ‘Ultrasound’ zinadanganya. Ilisema ana watoto wawili kumbe ni mmoja. Kwakweli hadi sasa sielewi,” ameongeza
0 maoni:
Post a Comment