Rais wa Tanzania Dkt. John
Magufuli amepokea barua yenye ujumbe wa Rais wa Jamhuri wa Rwanda Mhe.
Paul Kagame iliyowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum ambaye ni Waziri wa
Elimu wa Rwanda Dkt. Musafiri Papias Malimba.
Pamoja
na kupokea barua hiyo, Mhe. Rais Magufuli na Dkt. Musafiri Papias
Malimba wamezungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania
na Rwanda ikiwemo katika sekta ya elimu hususani maendeleo ya sayansi
na teknolojia.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza
Rwanda kwa kuamua lugha ya Kiswahili ianze kufundishwa katika shule zake
na ameahidi kuwa Tanzania ipo tayari kutoa walimu wa kwenda kufundisha
lugha hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Dkt. Musafiri
Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame
alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017. Wengine
ni Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura na Afisa Mwandamizi wa
Ubalozi Bw. Issa Mugabutsinze.
0 maoni:
Post a Comment