Polisi na mshambuliaji wauawa karibu na Champs Elysées


media Askari akitoa ulinzi kwenye mtaa wa Champs-Élysées na kumkataza mpita njia kusogea kwenye eneo la shambulio, Aprili 20, 2017. REUTERS/Benoit Tessier
Risasi zilipigwa kwenye saa tatu usiku siku ya Alhamisi, April 20 kwenye mtaa wa Champs Elysées mjini Paris, nchini Ufaransa. Polisi mmoja aliuawa, wengine wawili walijeruhiwa vibaya. Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, mshambulizi aliuawa kwa risasi. viongozi wanaona kwamba shambulio hilo ni la kigaidi.
Milio ya risasi ilisikika katika Ikulu ya Champs Elysées. Inaamika kuwa mshambuliaji au washambuliaji walifyatua risasi kwa silaha za kivita dhidi ya gari la polisi lililokua limeegeshwa katika moja ya mtaa wa mji wa Paris.
Polisi mmoja aliuawa na mwingine kujeruhiwa, yamearifu makao makuu ya polisi ambayo yanaomba raia kuepuka kutembelea eneo linalozingirwa na vikosi vya usalama
Hata hivyo polisi iliingilia kati na kufaulu kumuua mshambuliaji, imesema Wizara ya Mambo ya Ndani. Bado ni vigumu kwa sasa kujua hali halisi ya mambo kuhusiana na tukio hilo. Kwa saas polisiimezingira eneo latukio na bado inawatafuta washambuliaji wengine.
Wakati huo huo kundi la Islamic State limedai Alhamisi hii usiku kwa njia yachombo chake cha propaganda Amaq kwa limehusika na shambulio katika mtaa wa Champs Elysées ambapo polisi aliuawa na wengine wawili kujeruhiwa vibaya, huku mshambuliaji akiuawa kwa kupigwa risasi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment