Kampeni za kisiasa nchini Kenya kuanza rasmi Jumapili hii


mediaUhuru Kenyatta (Kulia), Raila Odinga (Kushoto) wanasiasa watakaopambana vikali katika uchaguzi wa urais mwezi AgostiDR.
Kampeni rasmi za kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti mwaka huu, zinaanza rasmi siku ya Jumapili kote nchini humo.
Mgombea wa urais kupitia muungano wa upinzani NASA Raila Odinga, anatarajiwa kuidhinishwa na Tume ya Uchaguzi kabla ya kuzindua kampeni zake  jijini Nairobi.
Wachambuzi wa siasa nchini Kenya wanasema  hii ni fursa wa mwisho kwa  Odinga ambaye anawania urais kwa mara ya nne sasa kujaribu kuingia katika Ikulu ya Nairobi.
Odinga aliwania mwaka 1997, 2007, 2013 na sasa 2017.
Mwanasiasa huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 72, amekuwa akisema kuwa ushindi wake uliibiwa mwaka 2007 na 2013.
Wanasiasa wa upinzani nchini Kenya katika mkutano uliopita wa kisiasaRailaOdingaK
Rais Uhuru Kenyatta naye ataidhinishwa na Tume ya Uchaguzi siku ya Jumatatu na kuzindua kampeni zake rasmi.
Kenyatta anayewania urais kwa muhula wake wa mwisho, amekuwa akisema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, serikali yake imesaidia kuimarisha maisha ya wananchi, madai ambayo upinzani unakanusha.
Mbali na wagombea hawa wawili wanaorudiana kwa mara nyingine kama ilivyokuwa mwaka 2013, kuna wagombea binafsi na wengine zaidi ya 10 kutoka vyama vingine  wamejitokeza kutafuta uongozi wa nchi hiyo.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwa na naibu wake William Ruto baada ya kutangaza kuundwa kwa chama kipya cha JubileeKenya State House
Maswala muhimu yatakayojiri katika kampeni:-
Rais Uhuru Kenyatta anasema anataka kuendeleza rekodi anayosema ni ya maendeleo nchini humo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, reli ya kisasa na mradi wa umeme kuwafikia idadi kubwa ya wakenya hadi kijijini.
Kenyatta anajivunia ujenzi wa reli ya kisasa atakayoizindua wiki ijayo kutoka Mombasa hadi jiji kuu Nairobi.
Mradi huu unatarajiwa kurahihisha usafiri wa abiria na mizigo kati ya miji hiyo miwili.
Rais Kenyatta na mgombea mwenza wake ambaye ni Naibu rais William Ruto, wanatarajiwa kutumia mafanikio haya kujitafutia uungwaji mkono.
Hata hivyo, upinzani umeendelea kuishutumu serikali ya rais Uhuru Kenyatta kwa kujihusisha na ufisadi na kukopa fedha kupita kisiasi kutoka nje ya nchi.
Utovu wa usalama pia ni suala ambalo upinzani unasema serikali ya sasa imeshindwa kushughulikia.
Kundi la Al Shabab limekuwa likiwashambulia raia wa kawaida na maafisa wa usalama kama polisi na wanajeshi, tangu kuingia madarakani mwaka 2013.
Kupanda kwa gharama za maisha hasa siku za hivi karibuni uhaba wa unga wa mahindi na sukari.
Serikali imelazimika kuingilia kati na kuamua kununua mahindi kutoka nchini Mexico ili kuwawezesha wananchi kupata unga kwa bei nafuu.
Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema ushindani mkubwa wa kisiasa unatarajiwa kati ya rais Kenyatta na Odinga.
Siasa za Kenya bado hazijaegemea sera lakini zinaendelea kuegemea ukabila na ukanda.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment