Wahamiaji haramu wakijaribu kuingia Ulaya walikusanyika Tajura kituo cha Tripoli, May 9, 2017.MAHMUD TURKIA / AFP
Viongozi
wa nchi zilizostawi kiuchumi duniani G7 wanataraji kukutana na viongozi
wa bara la Afrika baadae kwa mazungumzo juu ya janga la wahamiaji.
Viongozi
kutoka Tunisia, Kenya, Ethiopia, Niger na Nigeria watazungumza na wakuu
hao katika siku ya pili ya mkutano wa G7 mjini Taormina, Sicily.Italia ilichagua kuwa mwenyeji wa mkutano huo ili kuvutia umakini kwa Afrika na mamilioni ya wahamiaji ambao wamekuwa wakihatarisha maisha yao kuelekea Ulaya.
Hata hivyo mjadala mkali ambao umeendelea kutawala vikao vya G7 ni kuhusu ugaidi na mabadiliko ya tabia nchi.
0 maoni:
Post a Comment