Matumaini
ya kupata manusura wengine baada ya kutokea kwa maporomoko ya ardhi
Kusini magharibi mwa China yanazidi kufifia wakati huu idadi ya watu
ambao bado hawajulikani walipo ikitajwa kuwa 118
Waokozi
wamefanikiwa kupata miili 15 kutoka kwenya mabaki ya miamba
iliyoafunika nyumba 62 huko Xinmo , kijiji chenye milima kilicho jirani
na mto jimboni Sichuan.
Maporomoko hayo ya ardhi yaliyotokea majira ya asubuhi siku ya Jumamosi na yanaaminika kuchochewa na mvua kubwa .
Manusura watatu pekee mtu na mkewe na mtoto wao wa mwezi mmoja , ndio wamepatikana wakiwa hai tangu mvua kubwa kusababisha kuanguka kwa upande mmoja wa mlima mapema jana Jumamosi.

0 maoni:
Post a Comment