Rais Obama atangaza kutoa kikosi kuisaidia Nigeria |
Rais Barack Obama ameshutumu utekaji nyara wa wasichana hao na kusema kuwa mataifa yanapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kulikomesha boko Haram.
Tayari tumetuma kundi letu Nigeria wamekubali msaada wetu ambao unashirikisha wajeshi,wadumishaji wa sheria na mashirika mengine ambao wanajaribu kutambua waliko wasichana hawa ili wawape msaada Rais Obama alisema.
Rais Obama amesema kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kukataa utekaji wa kikatili wa wasichana hao kama msingi wa kuungana.na kuangamiza Boko Haram.
0 maoni:
Post a Comment