Licha ya kukabiliwa na marufuku ya FIFA kwa miezi minne kwa kumng'ata mlinzi wa Italiy Giorgio Chiellini Barcelona ya Uhispania aijakata tamaa ya kumsajili mshambuliaji machachali wa Uruguay luis Suarez.
Mshambuliji huyo tegemeo wa kilabu ya Livepool ya uingereza amepigwa marufuku ya miezi minne kumaanisha kuwa atoshiriki mechi yoyote hadi mwezi Octoba.
Aidha Suarez atoweza kufanya mazoezi katika kipindi hicho.
Haijulikani kwa nini mabingwa hao wa zamani wa kombe la mabingwa barani uropa ambao ambao wanajivunia huduma za lionel messi wa Algentina na Neymar wa Brazil bado wanamtaka Suarez
Liverpool ilimnunua Suarez kwa pauni milioni 25m mwezi januari 2011 kutoka kilabu ya Ajax.
hii sio mara ya kwanza kwa mchezaji huyu kukabiliwa na hii kashfa kama hii ya vkuwauma wapinzani wake,msimu uliopita alilazimika kukaa nje kwa miezi 10 baada ya kupatikana na atia ya kumuuma mlinzi wa Chelsea Branslav Ivonovic April 2013
mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 27 alilejea kwa kishindo na kuifungia livepool mabao 31 na kuisaidia kumaliza kwa nafasi ya pili.
Suarez pia alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2013-2014
Nyota huyo wa Uruguay alipokelewa kwa shangwe ndelemo na vifijo katika uwanja wandege wa kimataifa wa Carrasco huko montevideo alkipo lejea nyumbani kutokja brazil.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment