WAGONJWA WA EBOLA WATOROKA HOSPITALINI.

Serikali ya sierra leone imeonya kuwa ni hatari kumpa hifadhi mtu yeyote aliye ambukizwa virusi vya Ebola.

hii ni baada ya taarifa kuwa baadhi ya wagonjwa wametoroka Hospitalini na kujificha.

kwa mujibu wa wizara ya afya nchini humo,baadhi ya wagonjwa wenye homa kali wametoroka hopitalini katika wilaya ya kenema,kitovu cha mlipuko wa ugonjwa huo.

shirika la afya duniani WHO limetoa wito wa araka kwa kuchukua hatua za haraka kudhibiti homa hiyo katika ukanda wa Afrika magharibi ambapo hadi sasa wagonjwa 400 wamefariki

mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo ndio mkubwa zaidi kushuhudiwa hasa kwa kuwa ndio umesababisha vifo vingi na kuenea zaidi nchi nyinginezo za kanda hiyo.

visa zaidi ya 600 vya ugonjwa huo vimeripotiwa nchini Guinea ambako ulianza miezi 4 iliyopita na katika mataifa jirani ya sierra leone na liberia.

Takribani asilimia 60 walioambukizwa ugonjwa huu wamefariki dunia



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment