BRAZIL YAIANGUSHA CHILE KUPITIA PENALTI

Chile walikuwa kalibu kuwasababishia wenyeji maafa,lakini selecao walinusulika baada ya bahati kuwaendea katika mikwaju ya penalti na kuingia robo fainali ya kombe la Dunia ambapo watakutana na Colombia.

Baada ya kuponea katika kundi D  pamoja na Uholanzi na Uhispinia,Chile ilionekana ndio timu inayoweza kusababisha usumbufu sana dhidi ya mpinzani yeyote,na ilitalajiwa kuwaangusha wenyeji Brazil.Lakini selecao walianza mechi huku wakifyatua risasi moto moto ilikuwaonyesha Laloja kuwa matumaini yeyote ya kuwaangusha yangegonga ukuta.

Brazil ilikuwa imekosolewa kwa kukosa mshikamano kwenye timu pamoja na mkakati lakini washambuliaji wa Brazil Neymar,Hulk na Fred- kila mala walikuwa wanawasumbua mabeki watatu wa chile.Selicao walichanganya pasi ndefu na fupi kwa wakati mmoja na kuwaacha wapinzani wao wakihema mjini Belo Horizonte.

Ukulasa wa magoli ulifunguliwa hata hivyo dakika ya 18,Neymar ali chonga Freekick , ambayo ilipigwa kichwa na Thiago silva,na Gonzolo jara akafunga goli katika lango lake . Akukuwa na mbinu nyingine ambayo Jara angetumia David Luiz alikuwa nyuma yake ambapo angeweza kufunga kirahisi.

Brazil iliendelea kutengeneza nafasi ,lakini ilikuwa zamu ya la Loja kusawazisha katika dakika ya 32 . Hulk aliupoteza mpira na Alexis Sanchez akawa tayali kumalizia mambo.Goli hilo alikutalajiwa ,lakini lilimkumbusha kila mmoja katika uwanja wa Estadio Mineiro kuwa Chile wanaweza kuwa wapinzani Hatari sana.

katika kipindi cha pili Chile ililekebisha makosa yao katika safu ya ulinzi na kuanza kumiliki  mpira na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga magoli.katika dakika ya 55 Hulk aliukamata mpira na kufunga goli,lakini likakataliwa baada ya refa aliamua kuwa aliunawa makusudi na akapewa kadi ya njano mara baada ya jina lake kuwa kwenye Orodha ya waliofunga magoli.

Dakika 90 zilikamilka baada ya kuwa 1-1 dakika 30 za ziada azikuwa na nafasi za kufunga magoli ,kwa sababu wachezaji walikuwa wamechoka miguu  lakini Mauricio pinilla Nusra awape ushindi Chile lakini kombola lake lilikuwa juu kidogo tu..... milimita kidogo na likagonga mwamba likarudi uwanjani

Ukafika wasaa wa mikwaju ya penalti na baada ya penalti nne kila timu mambo yakawa 2-2 Neymar alijitokeza na kumbwaga kipa Bravo.Jara akajipa ujasili wa kupiga penalti ya Chile  lakini akakosea na mpira ukagonga mlingoti  hivyo Brazil walifuzu baada ya magoli 4-3.



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment