PODOLSKI KUKOSA MPAMBANO ZIDI YA ALGERIA

Lukas podolski atakosa mchuano ujao wa kufuzu katika robo fainali dhidi ya Algeria utakao chezwa Jumatatu (30.06.2014).kocha Joachim Low pia amesema beki Jerome Boateng bado ayuko "fiti"

low amewaambia waandishi wa Habari katika kambi ya mafunzo ya ujerumani Santo Andre kuwa podolski atakuwa tayari kwa wakati unaofaa kucheza bmpambano wa Algeria,akisema kuwa mchezaji huyo wa pembeni wa ARSENAL atastahili kupumzika kwa siku mbili au tatu.

Kocha huyo wa ujerumani amesema "inaweza kuwa hatari kubwa"kumjumuisha podolski kikosini katika mpambano huo wa jumatatu ,kwa sababu unaweza kuhathili jeraha lake hata zaidi.anaweza kuwa  tayali kwa mechi nyingine ikiwa watafuzu.

Beki Jerome Beateng amepata jeraha jingine mara hii akiumia katika goti lake la kushoto .low amesema jeraha hilo sio baya sana.

Dhidi ya Algeria ,Low  amesema Ujerumani inapambana na timu dhabiti zaidi ya Afrika katika dimba hilo kufikia sasa.amesema Dessert warrioris ni" hatari mno na wenye nguvu uwanjani" na hivyo haitakuwa kazi lahisi kwa vijana wake

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment